MAJALIWA AWATAKA MADIWANI KUMALIZA TOFAUTI ZAO ZINAZOKWAMISHA UTENDAJI WA KAZI

Waziri mkuu kassim majaliwa atoa siku mbili kwa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya kyela mkoani mbeya kumaliza tofauti zao zinazokwamisha utendaji wa halmashauri hiyo na kuendelea kufanya kazi walizotumwa na wananchi.
Tofauti hizo ambazo zimedumu kwa takriban mwaka mmoja zmesababisha madiwani hao kushindwa kufanya vikao jambo linalokwamisha shughuli za maendeleo ya wananchi katika halmashauri hiyo.
waziri mkuu ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya kyela akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani mbeya amesema ni lazima madiwani hao kumamaliza tofauti zao na wawaite wakuu wa idara na kuwapa taarifa hiyo ili shughuli za maendeleo ziendelee kutekelezwa ndani ya halmashauri hiyo.
amesema baadhi ya madiwani hao wanawatetea watumishi waliosimamishwa kazi kwa tuhuma za kuiibia serikali mabilioni ya fedha jambo ambalo halikubaliki na halivumiliki.
Hata hivyo, waziri mkuu ameiagiza taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa (takukuru) mkoa wa mbeya kuhakikisha watumishi wote waliohusika katika kula fedha za umma wanachukuliwa hatua kama alivyopendekeza mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali(cag).
pia aliwahasa watumishi wa umma kuhakikisha wanatimiza wajibu na majukumu yao kikamilifu kwa kufanya kazi kwa bidi na kuacha ubabaishaji na kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wawahudumie wananchi ipasavyo.