MAJENGO YA KIHISTORIA YANAUWEZO WA KUCHANGIA UKUAJI WA UCHUMI NCHINI

 

Majengo ya kihistoria yanauwezo  wa kuchangia ukuaji wa uchumi nchini endapo yatatumiwa ipasavyo.

Akielezea  historia ya nyumba hizo  huko maruhubi baada ya kutembelewa na ujumbe kutoka oman   abdalla khamis ali  mkuu wa kitengo cha mambo ya kale amesema  ni vyema majengo hayo yakaimarishwa zaidi ili kuwa kivutio kwa watalii waanaoingia nchini na kuleta mafanikio  mbali mbali .

Amesema kuongezeka kwa watalii kutasaidia wananchi wa zanzibar  kupata ajira na kupelekea kukuwa kwa pato la nchi.

Aidha mawasisitiza  wananchi kuwa na utamaduni wa  kutembelea majengo ya kihostiria ili kujua historia ya nchi yao   na kutoa elimu kwa kizazi kijacho.

Nae mwenyekiti wa taasisi ya nyaraka kutoka omani  heme d al-dhawiyan amesema ni vyema  mashirikiano yliyokuwepo kati ya oman na zanzibar yakadumishwa ili kuendelaza     biashara  katika maeneo ya kihistoria .

Ujumbe huo umetembelea maeneo mbali mbali ya kihistoria ikiwemo  maruhubi .mtoni na kijichi.