MAJESHI YA IRAK YASHAMBULIA MAGAIDI WA IS NDANI YA SYRIA

 

Majeshi ya serikali ya Irak yameingia katika kitongoji cha Mosul Magharibi kwa mara ya kwanza tangu yalipoanzisha operesheni ya kuukomboa mji wa huo kutoka kwa magaidi wanaojiita Dola la Kiislamu IS. Majeshi ya Irak yameiteka sehemu hiyo siku moja baada ya kuukomboa uwanja wa ndege wa mji wa Mosul uliokuwa unashikiliwa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la IS. Baada ya kutimuliwa kutoka Mashariki mwa Mosul, magaidi hao wamejichimbia katika sehemu ya Magharibi ya mji huo. Wakati huo huo, Waziri mkuu wa Irak Haidar al-Abadi amesema kuwa Jeshi la anga la nchi yake kwa mara ya kwanza liliwashambulia wanamgambo wa Dola la Kiislamu katika nchi jirani ya Syria