MAJESHI YA WAKURDI WAKO KATIKA NAFASI NGUMU YA KUOMBA MSAADA

 

Majeshi ya wakurdi yanayojaribu kupambana na mashambulizi ya majeshi ya uturuki kaskazini mwa syria wako katika nafasi ngumu ya kuomba msaada kutoka katika utawala ambao wanataka mamlaka zaidi ya ndani.

Utawala uliojitangaza wenyewe wa wakurdi katika eneo hilo umeyataka majeshi ya rais bashar al-assad kulinda eneo lao la afrin, ambalo majeshi ya uturuki yakisaidiwa na waasi wa syria walilishambulia januari 20.Lakini wakurdi katika eneo hilo wanakataa masharti ya serikali ya syria ya kurejesha majeshi ya serikali kuu na taasisi zake katika jimbo hilo.Hatua kama hiyo itafikisha mwisho udhibiti wa wakurdi katika jimbo la afrin, moja kati ya majimbo matatu ambayo yametangazwa na uongozi wa wakurdi, yaliyoko katika mpaka na uturuki