MAJIMBO TAJIRI KASKAZINI MWA ITALIA YAMEPIGA KURA KUPEWA MAMLAKA ZAIDI

 

Majimbo mawili kati ya majimbo tajiri zaidi ya kaskazini mwa italia yamepiga kura kupewa mamlaka zaidi, katika kura mbili za maoni zilizofanyika katika majimbo  hayo, wakati huu ambapo jimbo la catalonia, linashinikiza kujitenga na uhispania.

Wapiga kura katika majimbo ya veneto, wameshiriki kwa wingi kuunga mkono kanuni ya mamlaka zaidi kugatuliwa kutoka serikali kuu ya mjini roma.

Kura hizo hazifunganishi kisheria lakini zinawapa viongozi wa majimbo hayo mawili udhibiti wa kisiasa watakapoanzisha majadiliano na serikali kuu juu ya ugatuzi wa madaraka kutoka roma kwenda majimboni.