MAKABURI YALIYO NA MAMIA YA WATU WANAOSADIKIWA KUWA NI WAHANGA WA MAUAJI YAGUNDULIKA

Makaburi ya pamoja yaliyo na mamia ya watu wanaosadikiwa kuwa ni wahanga wa mauaji yaliyofanywa na wanamgambo wa kundi linalojiita dola la kiislamu is yamegunduliwa katika kambi ya zamani ya jeshi iliyoko kaskazini mwa iraqi.
Kaimu gavana wa kirkuk amesema kiasi ya miili ya watu 400 imegundulika katika kambi ya al-bakara karibu na hawija na gavana huyo ameitaka serikali ya iraq na umoja wa mataifa kuyaangalia makaburi hayo ili kuwatambua wahanga hao.
Operesheni za kuukomboa mji wa hawija kutoka kwa wanamgambo wa is zilianzishwa mwezi septemba na hadi kufikia mwezi oktoba waziri mkuu wa iraq haider al-abadi ametangaza kukombolewa kwa mji huo kutoka mikononi mwa kundi hilo.