MAKAMBA AMEVUNJA BODI YA BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA NEMC

Waziri wa nchi afisi ya makamu wa rais muungano na mazingira mh. Januari makamba amevunja bodi ya baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira nemc na kutengua uteuzi wa wajumbe saba wa bodi hiyo kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao.
mh. Makamba ameyasema hayo wakati alipokuwa akiongea na waandishi jijini dar es salaam amesema hatua hiyo waliyochukua ni kutokana na bodi hiyo kushindwa kusimamia dhamana ya utekelezaji wa majukumu yake.
amezitaja hatua nyengine alizo zichukuwa ni pamoja na kufanya marekebisho ya uongozi wa baraza hilo na kuwasimamisha kazi wafanyakazi wanne akiwemo mwanasheria mkuu wa baraza hilo ili kupisha uchunguzi kwa tuhuma zinazowakabili ikiwemo vitendo vya rushwa.
pia amesema wizara yake itaanzisha dawati la ujenzi kwa wawekezaji wa viwanda ili kutoa nafsi ya kupata ushauri wa mambo ya mazingira na kujenga katika maeneo yaliyopangwa.