MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AMESEMA ZANZIBAR INA MATUMAINI YA KUKUZA UCHUMI WAKE

Makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi amesema zanzibar ina matumaini ya kukuza uchumi wake kufuatia shirikisho la viwanda nchini india wa kuonyesha nia ya kuwekeza hasa katika miradi ya sekta ya kilimo.

Balozi seif ali iddi akiuongoza ujumbe wa viongozi wawili wa serikali
ya mapinduzi ya zanzibar katika ziara yake ya wiki moja
nchini india alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha pamoja kati ya
ujumbe wake na uongozi wa shirikisho la viwanda nchini india {cii}
hapo katika ukumbi wa hoteli ya kimataifa ya crowne plaza mjini kochikatika jimbo la kerala.
Alisema zanzibar bado inakabiliwa na ukosefu wa utaalamu wa kutosha katika kuendesha miradi inayotokana na kilimo cha viungo kiasi kwamba mapato yatokanayo  na kilimo hicho hayendi sambamba na nguvu zinazotumika.
Mapema katibu mkuu wizara ya kilimo, maliasili, mifugo na uvuvi nd.
Juma ali juma aliueleza ujumbe huo wa shirikisho la viwanda nchini
india kwamba kilimo bado kinategemewa kuwa muhimili wa uchumi wa zanzibar kilichoundiwa sera katika kuona kinamkomboa mwananchi hasa mkulima.
Alifahamisha kwamba serikali ya mapinduzi ya zanzibar inaendelea na
mipango ya kuimarisha sekta ya uvuvi katika bahari kuu ambayo bado
haijatumia ipasavyo ili iweze kutoa ajira nyingi zaidi kwa wazalendo.
Nd. Juma alifafanua kwamba bidhaa zitakazotokana na mazao ya baharini
zinaweza kutoa mchango mkubwa wa chakula katika sekta ya utalii nakuipunguzia mzigo serikali kuu bidhaa hizo kuagizwa nje ya nchi jambo ambalo huhitaji gharama kubwa ya fedha.
Kwa upande wake mjumbe wa baraza la wawakilishi ambae pia ni waziri asiye na wizara maalum zanzibar dr. Sira ubwa mamboya alisema kundi kubwa la wanawake na vijana wanaomaliza masomo yao ya sekondari bado wanahitaji kuungwa mkono.
Dr. Sira alisema kipato wanachokipata makundi hayo kwa sasa  katika
baadhi ya kazi wanazozifanya hakijaweza kukidhi mahitaji yao halisi ya kuendesha maisha yao ya kila siku.
Akitoa shukrani kwa niaba ya ujumbe wa shirikisho la viwanda nchini
india {cii} makamu mwenyekiti wa shirikisho hilo bwana george paul
aliueleza ujumbe wa zanzibar kwamba taasisi zilizo chini ya mwamvuli
wa shirikisho hilo zimepata shauku ya kuangalia namna zinavyoweza
kuelekeza nguvu zao za uwekezaji visiwani zanzibar.
Bwana paul alisema wapo wawakilishi wa kampuni za uwekezaji katika sekta ya biashara zinazotarajiwa kushiriki maonyesho ya biashara dar es salaam tanzania ambao wameamua kupanga utaratibu wa kiufika zanzibar kuangalia mazingira yaliyopo katika sekta ya uwekezaji vitega uchumi