MAKAMU WA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMEVIOMBA VYOMBO VYA SHERIA KUWACHUKULIA HATUA KALI

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh: Samia Suluhu hassan ameviomba vyombo vya sheria kuwachukulia hatua kali  watakaobainika kuwafanyia  vitendo vya udhalilishaji watu wenye ulemavu pindi makosa yao yakithibitika.

Amesema  kwa kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikiwakosesha amani jamii hiyo  hivyo amewataka watu wenye ulemavu na makundi mengine kushirikiana kikamilifu katika kupiga vita hali hiyo.

Mh samia ametoa agizo hilo katika maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani yaliyofikia kilele chake jimbo la uzini wilaya ya kati ambapo amesema serikali itaendelea kusimamia haki za watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kujumuishwa katika nafasi mbali mbali za uteuzi na majukumu mengine.

Akizungumza  katika maadhimisho hayo waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa Rais Mh: Mohd Abuod Mohd  ameitaka jamii   kushirikiana na watu wenye ulemavu kuhakikisha haki zao za msingi zinalindwa.

Katika  Risala yao watu wenye ulemavu  wamesema licha  ya  serikali zote mbili kuchukuwa juhudi za kutetea watu hao bado udhalilishaji umekuwa ukifanyika na kumekuwa na ucheleweshwaji wa kutolewa hukumu kesi zinazowahusu.

Katika maadhimisho   hayo makamu wa rais alikabidhi vifaa vya  baiskeli na fimbo kwa watu hao  wenye ulemavu.