MAKUNDI YA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM BADO WANAHITAJI KUUNGWA MKONO NA JAMII

Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya vijana ya wizara ya kazi, uwezeshaji, wazee, vijana, wanawake na watoto bibi mwanaidi mohamed ali amesema makundi ya watu wenye mahitaji maalum bado wanahitaji kuendelea kuungwa mkono na jamii katika njia ya kujaribu kukabiliana na changamoto zao.

Amesema njia hiyo ikiwemo misaada ya kibinaadamu, vifaa pamoja na taaluma zinaweza kuwa chachu ya kuwaondoshea fikra potofu za kujihisi kwamba wanatengwa na jamii iliyowazunguuka.