MALASYIA NA K.KASKAZINI ZALUMBANA KIFO CHA KIM JONG NAM

 

Korea kaskazini na malasyia kila moja imezuwia raia wa kutoka nchi nyingine kuondoka katika nchi hizo katika mzozo unaohusu mauaji ya kim jong-nam.

Hatua hizo kali za kulipiza kisasi zinachukuliwa wakati korea kaskazini ikikasirishwa na uchunguzi wa malasyia unaoendelea kuhusu kifo chake kilichotokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa kuala lumpur.

Malaysia haijailaumu moja kwa moja korea kaskazini kwa kifo hicho, lakini inashukiwa kwa kiasi kikubwa kwamba serikali ilihusika.

Katika hatua nyengine malaysia inataka iachiwe huru raia wake wanaozuiliwa nchini korea kaskazini.