MALENGO MAHUSUSI YA KITAASISI NA UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA JAMII.

 

 

Mabaraza ya wafanyakazi katika sehemu za kazi yametajwa kuwa chachu ya kufikia malengo mahususi ya kitaasisi na utoaji wa huduma bora kwa jamii.

Akizungumza baada ya kufungua kikao cha tano cha baraza la tano la wafanyakazi wa  mamlaka ya mkemia mkuu wa serikali,  mganga mkuu wa serikali profesa mohamed bakari kambi kwa niaba ya katibu mkuu wizara ya afya , maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto amesema  mabaraza ya wafanyakazi ni muhimu katika kuwezesha mafanikio.

Amesema madhumuni ya mabaraza la wafanyakazi ni kutoa fursa kwa watumishi kupitia wawakilishi wao  katika kujadili tija na ufanisi kwa upande mmoja na upande mwingine kuishauri menejimenti juu ya maslahi yao kama inavyoainishwa  katika sheria ya majadiliano ya pamoja katika utumishi wa umma  sura no 105

Naye mkemia mkuu wa serikali dkt fidelis mfumuko amesema kuna uhusiano mzuri kati ya taasisi na baraza  wafanyakazi ambapo  baraza hilo lilitoa  ushauri katika ununuzi  wa vifaa vya mamlaka ikiwemo mitambo mbalimbali   inayotumika katika  uchunguzi wa kimaabara na pia kutoa ushauri katika uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi.

Baraza hilo  pia limelenga  kujadili miongozo mbalimbali ya uendeshajin wa shighuli za mamlaka, taarifa ya utekelezaji ya nusu mwaka kupokea mada zinazohusiana na  kituo cha  kudhibiti matukio  ya sumu  ,utunzaji kanzi data pamoja na  kujadili hoja zinazowasilishwa na chama cha wafakazi wa mamalaka yaani tughe