MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA TCRA KUENDELEA KUTOA ELIMU JUU YA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAONI

 

Mwenyekiti wa kamati ya ardhi na mawasiliano ya baraza la wawakilishi Zanzibar hamza hassan juma ameitaka mamlaka ya mawasiliano tanzania tcra kuendelea kutoa elimu juu ya sheria ya makosa ya mtandaoni kwa upande wa Zanzibar ambapo imeonekana kuna ongezeko la matumizi mabaya ya mtandao hasa kwa vijana.

Amesema Zanzibar ipo sheria kama hiyo lakini utekelezaji wake umekuwa na changamoto ambazo zinapelekea kuwepo kwa makosa hayo na kuwepo kwa vitendo vinavyovunja utamaduni na silka za kizanzibar.

Nae naibu waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano mhandisi edwin ngonyani amewataka watanzania kutumia mitandao kwa ajili ya maendeleo na kutotumia kwa kufanyia uhalifu.

Wakitoa mada kamishna msaidizi wa jeshi la polisi andy mwakalukwa na naibu waziri wazira ya ujenzi, mawasiliano  na usafirishaji kutoka zanzibar mohd ahmada salum kwa pamoja walikuwa na haya ya kusema.

Kamati hiyo pia imetembelea  kampuni ya simu ya mkononi ya zantel na haloteli.