MAMLAKA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI IMEWAZAWADIA

 

Mamlaka ya mkemia mkuu wa serikali imewazawadia  fedha taslimu na vyeti  wanafunzi waliofaulu vizuri masomo ya kemia na bailojia kidato cha nne mwaka 2016 na cha sita mwaka 2017 .

Akizungumza katika hafla ya kuwazawadia wanafunzi waliofanya vizuri  mganga mkuu wa serikali profesa mohamed bakari kambi  amesema   ufaulu mzuri wa  wanafunzi katika masomo ya sayansi ndio suluhisho la changamoto ya upungufu wa wataalamu kwenye maeneo hayo.

Naye mkemia mkuu wa serikali dkt fidelis mfumuko amesema  mamlaka hiyo imeweka utaratibu huo ili kuleta chachu kwa wanafunzi  kupenda masomo ya sayansi.

Miongoni mwa waliozawadiwa ni mwanafunzi abu-bakar ali hassan  wa shule ya sekondari fidel-casto pemba ambaye alishika nafasi ya kwanza kwa somo la kemia kitafa, na amira mohamed  aliyeshika nafasi ya pili, nelda john kutoka marian girls nafasi ya 3 kemia kitaifa na paschal joseph wa shule ya sekondari kibaha aliyeshika nafasi ya pili kemia na nafasi ya tatu bailojia.

Zawadi hizo pia zikatolewa kwa  walimu bora wa sayansi waliowezesha ufaulu kwa wanafunzi.

nao wazazi wakapongeza utaratibu huo