MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA MAJI NA NISHATI ZANZIBAR ZURA IMETANGAZA BEI MPYA ZA MAFUTA

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za maji na nishati Zanzibar zura imetangaza bei mpya za mafuta kuanzia tarehe 12/12/2017.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika ofisi za mamlaka hiyo maisara mjini zanzibar kaimu mkurugenzi huduma kwa wateja nd. Mussa ramadhani haji ameeleza kuwa zura inapanga bei kwa kuzingatia mambo yafuatayo ikiwemo wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta duniani katika mwezi wa novemba 2017 kwa lengo la kupata kianzio cha kufanyia mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi disemba 2017, thamani ya shilingi ya tanzania, gharama za usafiri hadi Zanzibar, bima, kodi za serikali na kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na reja reja.

Kaimu mkurugenzi huyo amefafanua kuwa bei ya reja reja ya mafuta ya petroli imepanda kwa shilingi 100  kwa lita kutoka shilingi 2130 mwezi novemba 2017 sawa na ongezeko la asilimia 4.5%.

Bei hizo mpya za mafuta zitaanza kutumika rasmi kuanzia kesho tarehe 12/12/2017.