MAMLAKA YA USIMAMIZI WA UVUVI WA BAHARI KUU TANZANIA KUDHIBITI UVUVI HARAMU

 

Mamlaka  ya  usimamizi  wa  uvuvi  wa  bahari  kuu  tanzania, imesema  imejiandaa vyema  kudhibiti  uvuvi  haramu  kwa  ushikiano  na  nchi  jirani  zinazopakana  na  bahari  ya  hindi.

Mkurugenzi  mkuu wa  mamlaka  hiyo nd. Hosea  gonza  mbilinyi, amesema  mamlaka imekuwa  ikishiriki  katika  doria  ya  baharini  na  angani  kwa  kutumia  zana  za  kisasa zenye uwezo  wa  kugundua  vyombo  vinavyovua  bila  kibali  katika  maeneo  ya  bahari  ya  tanzania.

Akizungumza katika  mkutano wa  jumuiya  ya  nchi  wanachama  zinazopakana  na  bahari  ya  hindi, amesema imekuwa  ikipata  mafanikio  kutokana  na  utaribu  wa  kubalishana  taarifa  juu  ya  mwenendo wa  shughuli  za  uvuvi  katika  maeneo  yao.

Mkutano  hhuo  ulioshirikisha nchi  21 wanachama  umefungwa  na  katibu  mkuu  wizara  ya  biashara, viwanda na  masoko zanzibar dk. Juma  ali  juma, ambae  amesema  mapendekezo  yaliyofikiwa  ya  kuandaa  mkakati  wa  kulinda  rasilimali  ya  bahari, itasaidia  kuimarisha  hali  ya  kiuchumi  kwa  wavuvi  wadogo  wadogo  katika  nchi  hizo.