MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA ZINAKABILIWA NA CHANGAMOTO KATIKA UJENZI NA UIMARISHAJI MIUNDOMBINU

Waziri mkuu kassim majaliwa amesema mamlaka za serikali za mitaa zinakabiliwa na changamoto mbalimbali katika ujenzi, na uimarishaji miundombinu ya barabara ikiwemo ya rushwa katika utoaji wa zabuni.
Amesema jambo hilo halikubaliki na kutaka kutokomezwa vitendo hivyo pamoja kukemea usimamizi hafifu wa mikataba ya ujenzi.
Akuzindua wakala wa barabara za vijijini na mijini (tarura) huko domoma waziri mkuu amewashauri watendaji wa taasisi hiyo kusimamia hayo na kuimarisha mtandao wa barabara za vijijini naili wananchi wengi kuitumia bila ya usumbufu na kukuza uchumi.
Akizungumzia vitendo vya baadhi ya viongozi wa halmashauri kubadilisha matumizi fedha za barabara ameagiza fedha zote zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya barabara kutumika kama ilivyopangwa.
waziri wa nchi ofisi ya rais-tamisemi, mh george simbachawene amesema tarura itakuwa kiunganishi muhimu kwa wananchi moja kwa moja hivyo kutasaidia katika kupata usimamizi bora wa miradi ya barabara.
Aidha ameiomba serikali mgawanyo wa mapato ya mfuko wa barabara uangaliwe upya ilikuweza kunufaisha pande zote husika.