JKU na Polisi zatoka sare ya bila kufungana

Timu za jku na timu ya polisi hii leo katika uwanja wa Amaan zimetoka sare bila kufungana katika mchezo Wa ligi kuu ya zanzibar mzunguko wa 11. Jku iliyovalia jezi nyekundu, ilionekana kucheza vizuri Lakini ilishindwa kuzitumia vyema nafasi walizopata Dhidi ya wapinzani wao.

Timu ya polisi nayo ilipata nafasi nzuri katika pambano Hilo lakini washambuliaji wake walionekana kukosa Shabaha kutumbukiza mabao golini. Ligi hiyo itaendelea kesho usiku kwa timu ya black Sailor kumenyana na mafunzo.