MANCHESTER UNITED NA ARSENAL KUFUDHU ROBO FAINALI

 

Michuano ya Efl Cup iliendelea usiku wa jana kwa manchester united na arsenal kufudhu katika robo fainali ya michuano hiyo,  shukrani kwa wachezaji makinda kuwabeba katika mechi hizo.

“Litle Eddie” hilo ni jina la utani la bwanamdogo Eddie Nketiah ambaye ana umri wa miaka 18 tu na jana Arsene Wenger alijaribu kumpa nafasi Nketiah katika mchezo  huo akitokea benchi.

Wakati Nketiah akipewa nafasi tayari Arsenal walikuwa wamelala bao moja lakini zikiwa zimebaki dakika 5 mpira kuisha isawazisha kabla yadakika ya 96 kuongeza bao lingine na kuwa mchezaji wa kwanza kufunga akiwa amezaliwa wakati Wenger ni kocha wa Arsenal.

Manchester United nao jana walikuwa na kiungo kinda aliyekichafua sana katikati ya uwanja Scott Mc Tominay, kiungo huyu alizaliwa Uingereza na klabu yake ya kwanza kuichezea ilikuwa Manchester United.

Alex Tuenzebe naye sio jina jipya , amezidi kudhihirisha ubora wake baada ya kiwango kizuri sana usiku wa jana na shukrani zimuendee Jesse Lingard kwa kufunga mabao yote mawili yaliyowavusha United.

Manchester City wakashinda kwa mikwaju ya penati huku .