MANISPAA KUENDELEA NA ZOEZI LA UKAMATAJI WA WANYAMA WANOZURURA MITAANI

 

Baraza la manispaa magahribi B limesema litaendelea na zoezi la ukamataji wa wanyama wanozurura ovyo mitaani ambao imekua ni kero kwa wakulima na watumiaji wa barabara hali inayopelekea kuondoa haiba nzuri ya mji.

Hatua hiyo imekuja kufuatia agizo la mkuu wamkoa mjini magharibi mh; ayoub moh’d mahmoud kwa kulitaka baraza la manispaa magharibi B kuondoa wanyama wanaozurura ikiwa ni miongoni mwa malalamiko ya wanachi wa jimbo la dimani walioyatoa kwa mkuu wa mkoa huo.

Akizungumza katika zoezi la ukamataji wa mbuzi na ngombe katika shehia ya bweleo na fumba  mkurugenzi manispaa magharirbi b Amour Ali Mussa amesema wafugaji wameacha tabia za kudhibiti wanyama wao hivyo hupelekea usumbufu kwa wakulima na watumiaji wa barabara.

Amesema wafugaji hawajakatazwa kufuga bali kinachotakiwa ni kuweka usimamizi mzuri ambao utawezesha kuwahudumia wanyama wake ipasavyo ili kuondokana na usumbufu wa kuharibu vipando vya wakulima pamoja na kukamatwa  kwa wanyama wao.

Msimamizi wa zoezi hilo iddi mbarak uledi amesema zoezi hilo limefganikiwa ipasavyo  hivyo ameitaka jamii ya wafugaji kuacha masula ambayo yatakua yanakwenda kinyume  na sheria jambo ambalo halikubaliki na kwamba baraza la manispaa magharibi B halitasita kuchukua hatua za kuwakamata wanyama wanaozurura ili kuvitokomesha vitendo hivyo.

Katika zoezi hilo jumla ya mbuzi 31 na ngombe 4 wamekamatwa na baraza la manispaa magharibi B  katika shehia ya bweleo na fumba.