MANISPAA MAGHARIB A LIMESEMA KUNA BAADHI YA WATU HAWAPO TAYARI KUPAMBANA NA MARADHI

baraza la manispaa magharib a limesema bado kuna baadhi ya wananchi hawajawa na mwamko wa kufuata  taratibu zinazotolewa na maafisa wa  afya  katika kupambana na maradhi ya kipindupindu.

akizungumza na waandishi wa habari juu uwepo wa wagonjwa waliogunduliwa kuwa na vimelea vya kipindupindu, mkurugenzi wa baraza la manispaa magharib  a  Said Juma  amewasisitiza wananchi  kuepuka kula au kunywa ovyo vyakula vya majimaji,kuweka mazingira safi na salama  katika  makaazi  kwa kuacha kutupa taka  ovyo.

amesema katika jitihada wanazochukuwa baraza limekagua nyumba  katika maeneo ya manispaa hiyo na kugundua jumla ya  nyumba 961 hazifuati taratibu za kiafya kwani baadhi yake hazina vyoo,nyengine hazina karo na baadhi hawatibu maji.

aidha  Nd said  amewataka wananchi kuunga mkono jitihada hizo kwa kuifanyia kazi taaluma wanayopewa juu ya kujikinga na maradhi hayo thakili  ili kuepuka  kuendelea kwa  waathirika wanaogundulika na vimelea vya  maradhi ya kipindupindu.

kufuatia taarifa iliyotolewa na wizara ya afya jumla ya watu  23 kutoka shehia  mbalimbali ikiwemo mtoni kidatu wamegundulika kuwa na vimelea vya maradhi hayo.