MAO TSE DONG UNATARAJIWA KUKABIDHIWA MWISHONI MWA MWEZI NOVEMBA

 

Uwanja wa michezo wa mao tse dong unatarajiwa kukabidhiwa    mwishoni  mwa mwezi novemba mwaka  baada ya ujenzi wake kukamilika.

Naibu waziri   wizara  ya vijana utamaduni sanaa na michezo lulu msham  amesema   uwanja huo ulichelewa kukabidhiwa wizara  kutokana na kuwepo uhaba wa saruji hali iliyojitokeza hivi karibuni

amehamisha kuwa   uwanja huo ambao hadi sasa wizara haijakabidhiwa   wizara husika nia ya serikali ni kuona unatumiwa na wananchi waolio wengi  pamoja  wakaazi wa  jimbo la kikwajuni  na maeneo ya jirani.

Naibu waziri alikuwa akijibu swala la mwakilishi wa jimbo la mfenesini machano othman saidi aliyetaka kujua   hatua  zilizofikiwa za ufunguzi wa   uwanja huo wa michezo.