MAOFISA KILIMO KUWA MAKINI KATIKA KUISAIDIA SERIKALI JUU YA UTEKELEZAJI WA MIPANGO YA MAENDELEO

Maofisa wa sekta ya kilimo, elimu na afya katika mkoa wa kusini unguja wametakiwa kuwa makini katika kuisaidia serikali juu ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa jamii.
Akizungumza ofisi ya mkoa tunguu kwa niaba ya katibu tawala mkoa, afisa mipango wa mkoa huo ndugu khamis rubea bukheti katika mafunzo ya kuwajenge uwezo wa kitaalamu juu ya uandaaji wa mipango, uchumi na matumizi sahihi ya fedha za umma katika kuwahudumia wananchi kwa maafisa na watendaji wa sekta tatu zilizogatuliwa mkoani humo.
amesema kwa vile maafisa wa sekta hizo ndio chachu katika kukuza uchumi wa taifa na maendeleo hivyo wanapaswa kuzingatia umuhimu wa kusimamia vyema mipango ya maendeleo katika ukusanyaji wa takwimu na taarifa sahihi kutoka kwa wananchi.
Akiwasilisha mada kuhusu uzalishaji katika kukuza uchumi afisa wa uchumi mkoni humo ndungu asma ali talib amesema ili kukuza uchumi wa nchi na kuleta maendeleo muongozo na upatikanaji wa taaluma zinahitajika kwa wananchi katika kuzlisha bidhaa zenye ubora hivyo ni vyema kwa maafisa kuwa karibu na wananchi.
Nao maofisa hao wamesema wameahidi kuyatumia vyema mafunzo yaliyoyapata sambamba na kuzisifu juhudi za serikali kwa kuanzisha mfumo huo kwani tayari umeanza kuleta mafanikio makubwa