MAONYESHO YA KILIMO YAMETOA MWAMKO MKUBWA KWA WAKULIMA NA WANANCHI

 

 

waziri wa mawasiliano miundombinu na usafirishaji dr. sira ubwa mamboya amesema      kwa kuwa maonyesho ya kilimo     yametoa mwamko mkubwa kwa wakulima na wananchi hivyo   yanahitaji kuendelezwa   na kuwa katika ushindani mkubwa  ifikapo mwakani.

amesema ikiwa wakulima watafanya hivyo yataweza kumuweka mkulima kupata kipato  chenye tija kutokana   na  uzalishaji wake.

dr sira ameeleza hayo wakati  akiyafunga maonyesho ya maadhimisho ya nane nane yaliyofikia kilele chake katika viwanja vya kizimbani  nje ya mji wa zanzibar.

amesema  serikali ya mapinduzi ya zanzibar imekuwa mstari wa mbele katika  kusimamia sekta ya kilimo kwa kuimarisha miundombinu    huku wizara ya kilimo ikiwa na juhudi ya kutoa elimu  kwa wananchi na mabwana shamba juu ya uzalishaji bora .

naibu katibu mkuu wizara ya kilimo mali asili mifugo  na  uvuvi  dr islam seif salum amesema wizara ya kilimo  imeamua kuandaa maonyesho hayo kwa lengo la kutoa fursa   kwa wakulima wadogo kujifunza  mbinu bora za uzalishaji, ukulima na uvuvi na kuleta mabadiliko ya sekta hizo nchini.

 akizungumza katika ufungaji wa maonyesho hayo waziri wa kilimo maliasili mifugo na uvuvi mh rashid ali juma amesema  maonyesho hayo ya mwaka huu yameweza kutoa mvuto  na kuingia katika ushindani  mkubwa  kwa wafanya bishara  hivyo yatakuwa endelevu.

kikosi cha jeshi la kujenga uchumi  jku zanzibar  ambacho ni miongoni mwa washiriki wa maonyesho hayo  kimekabidhiwa zawadi   baada ya kufanya vizuri zaidi ukilinganisha na taasisi nyengine

rais mstaafu wa jamhuri ya muungano wa tanzani mhe, ali hassan mwinyi  amesifu maonesho hayo bada ya  kuyatembelea.