MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

 

Mkuu  wa  mkoa  kusini  mh hassan  khatibu  hassan amesema  nguvu za  pamoja  zinahitajika katika kuongeza  kasi  ya  mapambano dhidi  ya  dawa  za kulevya ili  kuikinga jamii  na janga la matumizi dawa  hizo.

Akizungumza  katika  mkutano wa kamati  ya  ulinzi  na  usalama  ya  mkoa  huo wakiwa na  tume  ya kuratibu na  kupambana na dawa za kulevya  zanzibar   katika  kupanga   mikakati  ya  udhibiti  ya  uingiaji  wa  dawa  hizo amesisitiza  uadilifu  kwa  viongozi  na  watendaji  wakuu  wa  serikali  ili  kuiokoa  nchi  kuingia  katika  janga  hilo  litalosababisha  kukosekana  kwa  vijana  ambao  ni  rasilimali  pekee  ya  taifa.

Amesema  imefika  wakati  kuhakikisha jamii  inashiriki  ipasavyo  katika  vita hii  ili  kuweza  kutoa  taarifa   pindipo  wanapoona  uingiaji wa  wageni  na  mizigo  isiyofahamika ili kuijulisha uongozi  wa  shehia  kwa  kushirikiana na kamati  ya ulinzi na usalama kuweza  kuifanyia  kazi  haraka  iwezekanavyo.

Kwa  upande  wake  mkurugenzi  mtendaji  wa tume  hiyo kheriyangu mgeni  khamis amesema inaonesha bado  elimu  ya  sheria ya  dawa  za  kulevya  inahitajika kwa askari  wapelelezi wa  kesi  hizo ili  waweze  watekeleze  vile  inavyohitajika pamoja  na kuhakikisha  kidhibiti  kilichokamatwa kinakuwa  katika  mazingira salama hadi  siku  ya  hukumu  ya  kesi   hiyo.

Washiriki  wa  mkutano  huo  wameshauri kuundwa  mahakama  maalum  dhidi  ya  kesi  ya kesi  za  dawa  za  kulevya pamoja  na kuchukuliwa  hatua kali za  kisheria kwa askaria ataebainika  kutotoa ushirikiano  wa  muendelezo  wa  kesi  hadi  kuchangia  kufutwa  kwake  au  kutokukamilisha vielelezo.

Kutokana  na  kikao  hicho  wamekubaliana  maadhimisho  ya  siku  ya  dawa za kulevya juni 26  kufanyika  katika  wilaya  ya  kati  mkoa  kusini  unguja  kutokana  na wananchi  wake kuhamasika kwa  kutoa  taarifa na  kufanikiwa  kukamata  kiasi  kikubwa cha  dawa  za  kulevya.