MAPATO YATAONGEZEKA KWA MABARA YA MIJI KUBUNI MIRADI MBALI MBALI YA UTOWAJI WA HUDUMA

Naibu waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalum za smz mh. Shamata shaame khamis amesema utowaji wa huduma bora kwa wananchi hautafanikiwa iwapo mabaraza ya miji
Hayatoongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato.
Mh. Shamata ametowa kauli hiyo baada ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa eneo la maegesho ya magari tibirinzi na eneo la soko la michakaeni ambayo itakuwa vianzio vipya ya mapato vya baraza la mji wa chake chake.
Amesema mapato yataongezeka kwa mabara ya miji kubuni miradi mbali mbali ya utowaji wa huduma ili wapate fursa za kukusanya fedha kupitia shughuli zitakazofanywa na wananchi.
Akizungumzia mradi wa maegesho ya magari mh. Shamata amesema kutekelezeka kwa mradi huo ni kutowa matumaini kwa baraza hilo ya hatua kubwa ya utekelezaji wa maagizo ya rais ya kuongeza ukusanyaji wa mapato.
Akitowa maelezo ya miradi hiyo muhandisi wa baraza la mji wa chake chake ibrahim salim rashid amesema tayari wafanyabiasha wa mboga mboga wameshapeleka maombi ya kulitumia eneo la soko la michakaini.