MAREKANI IMEISHUTUMU KOREA KASKAZINI KUWA INATAFUTA VITA

Marekani imeishutumu korea kaskazini kuwa inatafuta vita kwa kila njia na kusema kuwa itafanya juhudi ili nchi hiyo iliyofanya jaribio la sita la kinyuklia iwekewe vikwazo vikali ingawa marekani inakabiliwa na pingamizi kutoka kwa china na urusi.
Balozi wa marekani katika umoja wa mataifa nikki haley ameliambia baraza la usalama la umoja wa mataifa katika mkutano wa dharura ulioitishwa hapo jana na marekani, uingereza, ufaransa, japan na korea kusini kuwa nchi yake itawasilisha azimio jipya la kutaka korea kaskazini kuwekewa vikwazo vipya katika kipindi cha siku chache zijazo.
Haley amesema vikwazo vikali ndivyo vitawawezesha kusuluhisha tatizo la korea kaskazini na wala sio njia ya kidiplomasia na kuongeza kuwa marekani haitaki vita na korea kaskazini lakini subira yao ina mipaka.