MAREKANI IMEPIGA KURA YA TURUFU KUPINGA AZIMIO LILILOUNGWA MKONO NA WANACHAMA WA BARAZA LA USALAMA

Marekani imepiga kura ya turufu kupinga azimio lililoungwa mkono na wanachama wengine 14 wa baraza la usalama la umoja wa mataifa ambalo lingemtaka rais donald trump kuubatilisha uamuzi wake wa kuitambua jerusalem kuwa mji mkuu wa israel.
Kura hiyo imeonyesha kiwango cha upinzani wa kimataifa dhidi ya uamuzi huo wa marekani.
Marekani ilitarajiwa kutumia kura yake ya turufu kulipinga azimio hilo lililotayarishwa na misri, lakini washirika wake wa kiarabu walitaka kura hiyo kudhihirisha kuwa nchi nyingine na hata washirika wengi wa marekani kama vile uingereza, ufaransa na japan zinapinga hatua ya trump.
Wapalestina walitangaza kutafuta azimio lenye masharti sawa na hayo katika baraza kuu la umoja wa mataifa lenye wanachama 193, ambako hakuna kura za turufu.
Lakini tofauti na baraza la usalama, maazimio ya baraza hilo kuu sio makubaliano ya kisheria, na ni israel pekee ndio iliyoiunga mkono marekani.