MAREKANI KUZIWEKEA WIKWAZO URUSI, IRAN NA KOREA KASKAZINI.

Baraza la wawakilishi la marekani limepiga kura kuweka vikwazo vipya dhidi ya urusi, iran na korea kaskazini.
Urusi inadaiwa kuingilia uchaguzi mkuu wa marekani mwaka jana, korea kaskazini na iran wameekewa vikw azo kufuatia majaribio ya makombora.
Muswada huo unatarajiwa kupitia kwa baraza la seneti kabla ya kupelekwa kwa rais trump ili uidhinishe na kuwa sheria kamili.
Mwenyekiti wa kamati ya mahusiano ya kimataifa ya bunge la urusi duma, leonid slutsky amesema hatua hizo mpya zitazorotesha uhusiano baina ya urusi na marekani.