Marufuku ununuzi wa sare za jeshi la zimamoto na uhamiaji

Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi mhe mhandisi hamad yusufu masauni amepiga marufuku ununuzi wa sare za jeshi la zimamoto na uhamiaji kwa taasisi binafsi na badala yake ameagiza sare hizo zizalishwe katika viwanda vya jeshi la magereza nchini. Naibu waziri masauni ameyasema hayo baada ya kutembelea kiwanda cha jeshi la magereza kilichopo ukonga kinachoendeshwa kwa nguvu kazi ya wafungwa ikiwa ni ufuatiliaji wa utekelezwaji wa agizo la rais wa jamhuri ya muungano la kulitaka jeshi hilo liwasimamie wafungwa katika uzalishaji wa sare, na shughuli nyinginezo za ujenzi na kubana matumizi. Naye kamishina wa magereza nchini dkt juma ali malewa amesema tayari wameshafanya mazungumzo na wakala wa ujenzi tbl pamoja na taasisi nyinginezo ili kutekeleza agizo hilo la rais magufuli alilolitoa wakati akiongea na maafisa wa jeshi hilo 29 novemba mwaka jana ambapo pia alilitaka jeshi la magereza kutotegemea kupatiwa ruzuku ya chakula cha wafungwa kutoka serikalini. Naye mkuu wa kiwanda cha magereza ukonga acp ismail mlawa amesema kiwanda hicho kilianzishwa mwaka 1952 kwa na lengo la kutoa ujuzi kwa wafungwa wanaotumikia kifungo cha muda mrefu. Naibu waziri masauni alitembelea pia mradi wa ujenzi wa nyumba za ghorofa kwa aajili ya makazi ya wafanyakazi unaojengwa na wakala wa ujenzi tbl kwa thamani ya shilingi bilioni kumi fedha zilizotolewa na rais magufuli na pia alitembelea ujenzi wa nyumba za gharama nafuu. Mapema mhandisi masauni aliianza ziara yake makao makuu ya jeshi la magereza.