MARUFUKU UPIGAJI DISCO,UUZAJI POMBE NA KUUZA VYAKULA WAKATI WA MCHANA

 

Mkuu wa mkoa wa mjini magharibi mh. Ayoub mohamed mahmoud amepiga marufuku upigaji disco,uuzaji pombe na kuuza vyakula wakati wa mchana isipokuwa hoteli za kitalii.

Amesema huo ni utaratibu wa kila ifikapo mwezi mtukufu wa ramadhani wa kuweka zuio hilo ili kuupa heshima mwezi huo.

Katika hatua nyengine mkuu huyo wa mkoa amewakumbusha watembeza watalii kuwaongoza wageni wao kuvaa mavazi ya heshima pamoja na wananchi kuheshimu utaratibu huo.

Pia amegusia wafanyabiashara kufuata taratibu za kibiashara kwa kutopandisha bei za bidhaa hasa zilizopata msamaha wa kodi.