MASHAMBULIZI YA ANGA YA SYRIA YAMEWAUA RAIA 230

 

Mashambulizi ya anga ya syria na urusi katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi yamewaua raia 230 katika kipindi cha wiki moja iliyopita ikiwa ni miongoni mwa mashambulizi mabaya ambayo yanaweza kuchukuliwa kama uhalifu wa kivita.

Kamishina mkuu wa shirika la haki za binadamu la umoja wa mataifa amesema ofisi yake imepokea taarifa ikiwa ni pamoja na picha za vidio zinazo onesha kuwa silaha za sumu zilitumika katika mashambulizi yaliyofanyika kwenye miji inayodhibitiwa na waasi.Amesema kutokana na hali hiyo hatua za ziada zinapaswa kuchukuliwa ili kuinusuru hali isizidi kuwa mbaya.Kamishna huyo amesema kwa kiwango ambacho mgogoro wa syria umefikia hivi sasa suala hilo linatakiwa liwasilishwe katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ikiwa ni pamoja na juhudi za kurejesha amani nchini humo.