MASHEHA KUFANYA UADILIFU KATIKA UGAWAJI WA MISAADA KWA WAHANGA WA MAAFA YA MVUA

Mkurugenzi wa kamisheni ya kupambana na maafa zanzibar Nd. Shaaban Seif, amewataka masheha kufanya uadilifu katika ugawaji wa misaada kwa wahanga wa maafa ya mvua ili kuepuka malalamiko.
Akizungumza wakati akikabidhi misaada katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya magharibi b amesema kuna baadhi ya masheha wamekua hawatendi haki wanapokabidhiwa dhamana hiyo na kutoa kwa wasiohusika.
Nd. Shaaban amefahamisha kuwa sheha yoyote atakaekwenda kinyume na agizo la ugawaji huo atachukuliwa hatua za kisheria.
Nao baadhi ya masheha waliopokea msaada huo wamesema watatekeleza jukumu hilo kwa mujibu wa taratibu huku wakiishukuru serikali kwa kuendelea kuwafariji walioathirika na maafa hayo.
akitoa shukurani kwa niaba ya waliofikwa na maafa amesema msaada huo utawapunguzia baadhi ya matatizo huku akishauri taasisi nyengine kuendelea kutoa misaada.
Misaada yote iliyokabidhiwa katika kamisheni ya kupambana na maafa kutoka kwa wadau mbalimbali ina thamani ya shilingi milioni thalathini na mbili na laki tano ambayo itagaiwa kwa awamu mbili.