MASHINDANO YA NAGE KUIBUA VIPAJI MBALIMBALI VYA WANAMICHEZO

 

 

Mashindano ya nage jimbo la mkwajuni yamefikia mwisho  huku  timu ya bado wazalendo imefanikiwa kuwa  mabingwa wapya wa michuano hiyo kwa mwaka huu 2018

Mashindano hayo yaliyoanza mwezi wa 6 mwaka huu yaliyokuwa  na  msisimko mkubwa kwa wanamichezo katika mkoa wa kaskazini unguja  kutokana na ushindani  mkubwa uliooneshwa na timu shiriki

Hatimae  mchezo wa fainali uliopigwa katika uwanja wa kibuyuni boys   wanadada wa timu ya bado uzalendo wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa michuano hiyo baada ya kuwashinda wanadada wenzao timu ya kibuyuni quein kwa ushindi wa chupa 7-4

Akizungumza na wanamichezo na viongozi katika ufungaji wa mashindano hayo mwenyekiti wa ccm mkoa wa kaskazini  iddi ali ame amewataka viongozi wa majimbo hasa mkoa wa kaskazini kuendeleza zaidi michuano kama hiyo ambayoimeonekana kuwa na muamko  kwa wanamichezo sambamba na utekelezaji wa ilani ya chama katika  kuibua vipaji mbalimbali vya wanamichezo

Naye mfadhili wa mashindano hayo mbunge wa jimbo la mkwajuni  khamis ali amesema michuano hiyo itakuwa endelevu na kila ifikapo  mwezi wa sita kila mwaka michuano hiyo itachezwa

Mabingwa wa michuano hiyo  timu ya bado uzalendo wamejishindia zawadi ya fedha taslim shilingi laki tatu na jezi seti moja, huku mshindi wapili kibuyuni quein akijinyakulia  shilingi laki mbili