MASHIRIKA YA KIMATAIFA YA MISAADA YAMEZIONYA NCHI ZA MASHARIKI YA KATI

 

Mashirika ya kimataifa ya misaada yamezionya nchi za mashariki ya kati pamoja na mataifa ya magharibi dhidi ya kuwarejesha kwa lazima wakimbizi wanaotoka nchini syria.

Ripoti iliyotolewa na mashirika ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na baraza la wakimbizi nchini norway na shirika la care international imesema, maelfu ya wakimbizi wako katika hatari ya kurejeshwa kwa lazima nchini syria katika kipindi cha mwaka huu wa 2018 licha ya vurugu zinazoendelea nchini mwao.

Ripoti hiyo iliyopewa kichwa cha habari cha mazingira ya hatari imesema ajenda ya kuwarejesha wakimbizi nchini syria inazidi kupewa umuhimu katika mataifa yaliyowapa hifadhi wakimbizi hao wa syria.Idadi ya wakimbizi waliorejeshwa nchini syria, nchi ambayo  inakabiliwa na mgogoro wa vita tangu mwaka 2011 ilipanda hadi kufikia laki 7 mwaka 2017 kutoka laki 5 mwaka uliotangulia.