MASHIRIKA YA KUTOA MISAADA YA KIBINAADAMU YAMEBAINI WATU AROBAINI WAMEUAWA

mashirika ya kutoa misaada ya kibinaadamu yamebaini watu zaidi ya arobaini wameuawa nchini jamhuri ya afrika ya kati, siku moja baada ya makubaliano ya kusitisha vita kati ya serikali na vikundi vya waasi.
mapema wiki hii mapigano makubwa yalitokea katika mji wa bria, ulioko kaskazini mwa mji mkuu, bangui.
mkataba wa amani nchini jamhuri ya afrika ya kati ulitiwa saini mjini roma, nchini italia ukijumuisha usitishwaji wa mapigano.
mkataba huo ulikua na lengo la kumaliza mapigano yaliyodumu miaka kadhaa yakihusisha vurugu kati ya wanamgambo wa kikristo na waislam.
jamhuri ya afrika ya kati imeendelea kukumbwa na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe kwa makundi mawili hasimu anti-balaka na seleka, kila upande yakidai kulinda jamii yake.