MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA YATAENDELEA KUISAIDIA SEKTA YA AFYA

 

Mashirika ya umoja wa mataifa yamesema yataendelea kuisaidia sekta ya afya hususan kwa afya ya mama na mtoto kwa lengo la kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.Mwakilishi wa shirika linaloshughulikia idadi ya watu duniani tanzania ndugu jaqline mahon amesema shirika lake limeandaa mpango maaluma wa kusaidia sekta ya afya pamoja na vijana ambao hawana ajira ili kuweza kujiari  mwenye. Amesema   mpango huo ambao utahkikisha kuwa kuna vifaa vya kutosha katika wodi za wazazi  kufanyia marekebsho majeng pamoja na kwapatia mafunzo madktari.Waziri wa afya mhe hamad rashid mohd amelishukuru shirika hilo na kusema wizara yake inathamini jitihada zinazochukuliwa na shirika hilo katika kuona afya za mama na mtoto zinaimarika na kuwawata wananchi kutumia uzazi wa mpango ili vifo vitokanavyo na uzazi viweze kupungu hapa nchini.