MASHITAKA ANAYETUHUMIWA KUENDESHA LORI NA KUWAGONGA WATEMBEA KWA MIGUU

 

Mashitaka ya ugaidi yamefunguliwa dhidi ya mtu kutoka uzbekistan mwenye umri wa miaka 29 anayetuhumiwa kuendesha lori na kuwagonga watembea kwa miguu mjini manhattan, amapo amewauwa watu wanane na kuwajeruhi wengine 12.

Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali amesema mtu huyo amehamasishwa na kundi linalojiita dola la kiislamu kuwashambulia watu siku ya jumanne.

Rais donald trump ameshutumu shambulio hilo, na kuliita kuwa ni tukio la kigaidi na ameamuru kuimarishwa hatua za kiusalama dhidi ya wahamiaji kufuatia shambulio hilo.

Mtuhumiwa, ambae polisi imesema alipanga shambulio hilo kwa wiki kadhaa, anaweza kukabiliwa na adhabu ya kifo kutokana na kesi iliyofunguliwa dhidi yake, na pia polisi imesema mtu mwingine pia anatafutwa ili kuhojiwa kuhusiana na shambulio hilo.