MATATIZO KATIKA USIMAMIZI WA MIKATABA

 

Kukabiliwa    kwa   kazi   nyingi  za   usimamizi  na  utendaji    kwa  wakati   mmoja  ni   mingooni  mwa  changamoto  zinazo zorotesha  ubora   na  umakini  kwa  wahandisi katika   kusimamia  mikataba  ya   ujenzi .

Washiriki   wa   mafunzo    ya   usimamizi  wa  mikataba   ya  ujenzi  yalioandaliwa  na   afisi  ya  mwanasheria  mkuu  wa   serikali  wamesema  hali  hiyo  imekuwa  ikiwapa    wakati  mgumu   katika   kutimiza   majukumu   yao   kama   inavyokusudiwa  kisheria .

Akitoa mafunzo hayo kwa  wanasheria wa serikali na wahandisi,mshauri muelekezi Ness Lemunge amesema kumekua kukijitokeza matatizo  katika usimamizi wa mikataba ikiwemo kufanya majadiliano ya mikataba hiyo, hivyo ni vyema kwa wasimamizi kuyatumia mafunzo hayo kwanjia ya kuleta mabadiliko ya  kiutendaji.

Mapema  akifungua mafunzo hayo ya siku nne  Mwanasheria Mkuu wa  Serikali Said Hassan Said amewasisitiza  watendaji hao  kufanya kazi zao kwa kufuata utaalamu watakaoupata na kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.