MATAYARISHO YA UJENZI WA KIWANJA KIPYA CHA NDEGE MAENEO YA KIGUNDA

 

Matayarisho ya ujenzi wa kiwanja kipya cha ndege katika maeneo ya kigunda mkoa wa kaskazini unguja yameanza kwa hatua ya kusafisha eneo hilo.

Hatua hiyo ya matayarisho imekuja baada ya mamlaka ya viwanja vya ndege zanzibar kukamilisha zoezi la kuwalipa fidia wananchi ambao walikuwa wanalitumia eneo hilo kwa shughuli za kilimo.

Kwa mujibu wa afisa uhusiano wa mamlaka  hiyo makame abdalla seti amesema matayarisho yameanza kwa hatua hiyo ya kusafisha uwanja kwa kuwatumia wakaazi wa vijiji vilivyozunguka eneo hilo kama ilivyoahidiwa hapo awali.

Amesema matarajio yanaonyesha kuwa hadi kufikia mwezi januari mwakani uwanja huo wenye ukubwa wa kilomita mbili utakuwa umeshaanza kutumika kwa hatua za awali ili kupanua wigo wa huduma za anga nchini.

Kwa upande wake afisa mazingira wa mamlaka hiyo suleiman hamad amehimiza ushirikiano wa wanavijiji pamoja na wananchi wengine kuona kuwa azma ya kuanza kwa ujenzi huo inatimia.