MATEMWE NA VIJIJI JIRANI KUTUMIA MAJI KWA UANGALIFU ILI KUNUFAIKA NA HUDUMA HIYO

Mamlaka ya maji zawa imewataka wananchi wa matemwe na vijiji jirani kutumia maji kwa uangalifu ili kunufaika na huduma ya maji safi na salama katika kijiji hicho.
akizungumza na wandishi wa habar afisa uhusiano kutoka zawa ndugu zahoro sleiman khatib amesema vijivi vitakavyofaidika na mradi huo wa maji ni vijiji vitano vikiwemo vya mikuu, mbuyumaji , kihogoni / jamba na mbuupopo.
Amesema mradi huo wa kisima cha maji una lita miatano kwa saa na umegharimu zaid ya shilingi milioni ishirini na nane.ikiwa ni juhudi za serikali kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma bora za maji safi na salama.
Naye mjumbe wa sheha hiyo ya ndugu vuai makame vuai amesema walikua wakipata shida kwa kipindi kirefu kuyafuata maji katika sehemu ya mbali.
Kwa upande wa sheha wa sheia hiyo bwana vuai farahani vuai. Ameishukuru serikali ya mapinduzi ya zanzibar kwa kuwajali wananchi wa matemwe kwa kuwapatia huduma muhimu.