MATEMWE WAMEIOMBA IDARA YA MAENDELEO YA UVUVI KUWEKA UTARATIBU MZURI WA UFUNGUAJI WA PWEZA

 

Wavuvi wa pweza na kamati ya wazee ya kijiji cha matemwe wameiomba idara ya maendeleo ya uvuvi kuweka utaratibu mzuri wa ufunguaji wa pweza ili kuondosha  mizozo  kati yao na wavuvi wa mzuri ambao walikaidi agizo  hilo.

Wamesema  wamekuwa wakipokea  maneno ya kashfa ya mara kwamara kwa  baadhi ya wavuvi hao juu ya ufunguaji wa pweza hali inayoweza kuharisha usalama wa vijiji hivyo .

Wakizungumza katika kikao cha pamoja na watendaji wa idara hiyo, juu ya  ya ufunguaji wa pweza ambao umezua mzozo  kati yao na wavuvi wa makunduchi,wamesema wao awali hawakukataa kushirikiana na wenzao  katika ufunguaji bali wamechoshwa na kauli zisizo nzuri kwa upande wao  wakati wao wenyewe wavuvi wa makunduchi walikataa ufungaji huo.

Akitolea ufafanuzi wa malalamiko hayo huko mtende wilaya ya kusini, mkurugenzi idara ya maendeleo ya uvuvi mussa aboud jumbe amewataka wavuvi wa mtende kuwa na uvumilivu na kuahidi kuyafanyia kazi malalamiko yao huku akiahidi kuwa ufunguaji huo utasimamiwa vizuri na idara hiyo pamoja na uongozi wa mkoa ili  kuondosha migogoro.