MATENGENEZO MIUNDOMBINU YA MAENEO YA KIHISTORIA

 

Mamlaka ya usimamizi wa shughuli za kiutalii kisiwani pemba imeshauriwa kuifanyia matengenezo miundombinu ya maeneo ya kihistoria zikiwemo barabara za kuingilia katika maeneo hayo ili kuwarahisishia wageni kufika katika maeneo hayo.

Ushauri huo umetolewa na mtalii mtembea bara la afrika kwa pikipiki maheir khalid al –barwan kwa nyakati tofauti katika safari ya kutembelea maeneo ya kihistoria kisiwani pemba

Amesema maeneo mengi yamekuwa yamejificha na hayafikiki kwa urahisi hivyo mamlaka lazima zitilie mkazo usimamizi kurejesha haiba ya maeneo hayo na kufika kwake.

Naye mkuu wa idara ya mambo ya kale khamis ali juma amesema katika kuliona hilo mamlaka kwa kushirikiana na serikali kuu imeandaa mpango wenye mkakati mkuu wa kuyaendeleza mambo ya kale katika hali zake zote ikiwemo urejeshaji wa baadhi ya majengo na barabara zake.