MATENGENEZO YA HARAKA BARABARA ZILIZOHARIBIKA KUFUATIA MVUA ZINAZOENDELEA.

Madereva    katika   Manispaa ya Zanzibar wameomba kufanyiwa matengenezo ya haraka barabara zilizoharibika kwa mashimo kufuatia mvua zinazoendelea.

Wamesema kuwepo kwa uchakavu wa barabara hizo unaosababishwa  na  mashimo  mengi katika barabara hizo ni kero kubwa wanapokuwa katika harakati zao za kila siku.

Baadhi ya barabara za mji wa zanzibar zimelalamikiwa kwa kuleta usumbufu kwa watumiaji kutokana na kushindwa kufanyiwa matengenezo ya uhakika sehemu zilizoharibika.

Zbc imeshuhudia barabara nyingi za mjini zikiwa katika hali mbaya ikiwemo ya kijangwani, saateni,kisonge na mwembeladu ambazo nyengine zimetuama maji ya mvua .

Mbali ya malalamiko hayo ya madereva wananchi nao wameelezea athari  wanazozipata kutokana  na kadhia hiyo ambayo pia wameelezea kupoteza haiba ya mji wa zanzibar.

Katika kufuatilia zaidi zbc ilifika hadi idara ya ujenzi na utunzaji wa barabara ( uub) ambapo taarifa zilishindwa kupatikana kwa urahisi