MATENGENEZO YA MAKUMBUSHO KUU YA JUMBA LA BEIT EL JAIB LILIOPO FORODHANI

 

Jumla ya dola milioni tano za marekani zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya kuifanyia matengenezo makubwa makumbusho kuu ya jumba la beit el jaib liliopo forodhani , kwa ufadhili wa serikali ya oman.

Hatua hiyo ya ujenzi inafuatia kukamilika kwa ziara ya ujumbe kutoka oman ulipofanya ukaguzi katika jumba hilo, ikiwa ni makubaliano kati ya serikali ya oman na serukali ya mapinduzi ya zanzibar.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari  katika jumba hilo, waziri wa habari, utalii na mambo ya kale, mh. Mahmoud thabit kombo, amesema  ujenzi huo utakaochukua kipindi cha miaka miwili kukamilika unatarajiwa kuanza muda mfupi ujao na kwamba vifaa kwa ajili ya ujenzi huo vinatarajiwa kuwasili baada ya wiki tatu.

Aidha amesema kuwa makubaliano ya ujenzi huo ni kulifanyia matengenezo jumba lote ili lilwe la kisasa na kwamba mafundi wenye utaalamu wa ujenzi wa nyumba za jiwe watarajie kupata nafasi baada ya kuthibitishwa na wataalamu wanaosimami ujenzi huo.

Akizungumzia juu ya ujenzi huo katibu mkuu wa wizara ya uhifadhi wa mambo ya kale wa oman  bw salim mohamed al mahruki, amesema anaimani kuwa kuimarika kwa jumba hilo itasaidia kuongeza pato la serikali ya zanzibar kwani imekuwa ni kivutio kikuu kwa watalii wanaotembelea zanzibar, lakini pia kutazalisha ajira kwa vijana.

Ujumbe huo wa oman umekamilisha ziara ya siku tano hapa zanzibar.