MATOKEO MABAYA YA WANAFUNZI YAMECHANGIWA NA WALIMU WALIOSHINDWA KUWAJIBIKA

Wazazi wa wanafunzi wanaosoma skuli ya msingi na sekondari ng’ambwa, wamesema matokeo mabaya ya wanafunzi kwa mwaka 2018, yamechangiwa na walimu ambao wameshindwa kuwajibika pamoja na kuwatolea maneno ya jeuri wazazi wanapofuatilia maendeleo ya watoto wao.

Matokeo mabaya ya mitihani ya taifa katika skuli hiyo yamewafanya wazazi kukutana kujadili mbinu na mikakati ya kuongeza idadi ya ufaulu ambapo mzee haji hamad kombo na robart miguwa pamoja na katibu tawala wilaya ya chake chake omar khamis juma wamesema ujeuri wa walimu pamoja na kukosa uzalendo ndio sababu ya matokeo hayo.

afisa elimu na mafunzo ya amali wilaya ya chake chake , abadalla omar muya amewataka walimu kuandika barua kujieleza na kuzifikisha ofisini kwake si zaidi ya siku ya jumatano, huku mwalimu asma ali hafidh akielezea kutoridhishwa na matumizi ya simu kwa wanafunzi.

Mkuu wa wilaya ya chake chake rashid hadid rashid akizungumza kwenye mkutano huo amewataka wazazi kumpa ushirikiano ili kufanikisha kudhibiti utoro wa wanafunzi.

Mkutano ni moja ya mkikati ya serikali ya wilaya ya chake chake kuhakikisha inadhibiti utoro wa wanafunzi na kuongeza ufaulu wa wanafunzi

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App