MATUKIO YA UKATILI NA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA.

Naibu katibu mkuu wizara ya kazi, uwezeshaj,i wazee, wanawake na watoto bi. Mwanajuma majid abdalla   amesema  hatua za makusudi za kuwaelimisha wananchi zinahitajika juu ya mpanngo maalum wa malezi ya dharura kwa watoto wanaohitaji ulinzi katika matukio ya ukatili na udhalilishaji wa  kijinsia.

Akifungua warsha ya siku tatu (3) ya kujadili mpango wa kukabiliana na malezi ya dharura (kambu) kwa timu ya wataalamu kutoka sekta mbali mbali  za masuala ya watoto amesema mpango huo ni muhimu kwa wakati huu ambapo zanzibar ina watoto wengi wanaohitaji huduma hiyo ya malezi.

Amesema watoto wengi wanakosa haki zao za msingi hivyo maafisa wa ustawi wa jamii na watendaji wengine  lazima kuangalia malezi mbadala ili yaendane na sheria, kanuni zil- izopo ili kuhakikisha watoto nchini wanalelewa katika vituo vinavyokubalika.

Mapema wakiwasilisha mada juu ya kanuni, muongozo,  na mpango wa malezi ya dharura maafisa wa hifadhi ya watoto kutoka idara ya wazee na ustawi wa jamii bi. Biubwa ali na mkasi abdulla wamesema malezi ya dharura ni malezi ya muda mfupi ama mrefu katika nyumba yatolewayo na mtu aliechaguliwa na idara hiyo iwapo  kuna sababu maalum ya kuunganishwa katika malezi hayo.