MAZIKO YA PAMOJA YA WATOTO WALIOFARIKI WAKIWA NDANI YA GARI

Wakaazi wa maeneo ya jang’ombe na maeneo jirani wamejitokeza katika maziko ya pamoja ya miili ya watoto waliofariki wakiwa ndani ya gari katika mtaa wa kidongo chekundu wilaya ya mjini unguja hapo jana.
Wakielezea kwa masikitiko wazazi wa watoto hao wamesema tukio la kupotea kwa marehemu waliwahi kutoa hao taarifa kwa vyombo mbalimbali na hatimae kungudua wamo ndani ya gari wakiwa wameshafariki baada ya juhudi kubwa ya kuwatafuta.
Kamanda wa polisi mkoa wa mjini magharibi hassan nassir, amesema wanaendelea na uchunguzi kwa kumuhoji mmiliki wa gari hilo ambae inasemekana alikuwa nje ya zanzibar.
Mkuu wa wilaya mjini marina joel thomas ambae aliambatana na waziri anaeshughulikia masuala ya watoto mh. Modeline castico . Wameeleza kusikitishwa na tukio hilo huku wakiwashauri wazazi kuwa makini kuwasimamia watoto ili maafa kama hayo.
Watoto waliofariki wametambulika kwa majina ya munawar ahmed khamis, muslim mohamed bakar, mwatima mohamed malau na haitham mustafa abubakar wote wakiwa na umri wa miaka miwili.
Tukio kama hilo limewahi kutokea dunga wilaya ya kati unguja na kusababisha vifo vya watoto watatu.