MAZISHI YA ALIYEWAHI KUWA KATIBU AFISI YA RAIS WA ZANZIBAR MAREHEMU MOH’D AHMADA

Makamu wa pili wa rais wa zanzibar, balozi seif ali iddi, ameungana na wananchi mbali mbali katika mazishi ya aliyewahi kuwa katibu afisi ya rais wa zanzibar, marehemu moh’d ahmada.
Dua na sala ya kumuombea marehemu zilifanyika katika msikiti nambari kisiwandui na mazishi yamefanyika katika makaburi ya mitondooni. Wakati wa uhai wake marehemu moh’d ahmada, aliwahi kushika nyadhifa mbali mbali serikalini ikiwemo katibu mkuu afisi ya rais wa zanzibar.
Katika mazishi hayo mshauri wa rais ushikiano wa kimataifa na uchumi,balozi moh’d ramia, aliekuwa mbunge jimbo la uzini, moh’d seif khatib pamoja na mshauri wa rais mambo ya utamaduni, chembeni kheir wameelezea jinsi wanavyomfahamu marehemu moh’d ahmada katika utendaji wake wa kazi.
Mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amin.