MAZUNGUMZO YA AMANI YA SYRIA YANAYODHAMINIWA NA URUSI YAMEANZA LEO

 

Mazungumzo ya amani ya syria yanayodhaminiwa na urusi mjini sochi, yameanza leo, licha ya makundi kadhaa ya upinzani yakiwemo ya wakurdi, yakisusia mazungumzo hayo.Miongoni mwa washiriki ni pamoja na serikali ya syria na watu wanaompinga rais bashar al-assad ambao si sehemu ya makundi yenye silaha yanayopigana na utawala wake.

Mjumbe maalum wa umoja wa mataifa nchini syria staffan de mistura amehudhuria mazungumzo hayo.Uturuki na iran zimetuma wawakilishi wao  katika juhudi za kutafuta amani iliyopotea nchini humo ambapo maelfu ya watu wamepoteza maisha na wengi wao kuyahama makaazi yao na kuingia katika janga la wakimbizi katika mataifa mbali mbali.